Saturday , 7th Jun , 2014

Shirikisho la ngumi za ridhaa nchini Tanzania BFT limesema mabondia wa Tanzania walioko nchi za China na Uturuki wakijiandaa na mashindano ya Jumuiya ya Madola yanayofanyika mwezi ujao nchini Scotland wamejigamba kurejea na medali.

Mabondia wa Timu ya Taifa ya Ngumi Tanzania Walivyo Katika moja ya mashindano ya ndani ya majaribio

Shirikisho la ngumi za ridhaa nchini Tanzania BFT limesema mabondia wa Tanzania walioko nchi za China na Uturuki wakijiandaa na mashindano ya Jumuiya ya Madola yanayofanyika mwezi ujao nchini Scotland wamejigamba kurejea na medali za dhahabu na shaba katika michuano hiyo mikubwa ya Dunia.

Akiongea mara baada ya kutoa msaada katika Zahanati ya Kawe jijini Dar es salaam, Rais wa BFT Mutta Rwakatare amesema mabondia watano walioko nchini China na watatu walioko nchini Uturuki wamejifunza kupambana kwa kasi tofauti na hapo awali walipokuwa wakitumia mbinu tofauti.

Akizungumzia sababu ya kutoshiriki katika michuano ya vijana ya Afrika chini ya umri wa mika 15 iliyofanyika mwishoni mwa mwezi Mei nchini Botswana, Rwakatare amesema walishindwa kupeke mabondia katika mashindano hayo kutokana na ukata wa fedha pamoja na kushindwa kuwagawa mabondia.

Kwa upande wake, mjumbe wa maendeleo ya michezo wa BFT, Aisha George amesema wanaandaa mashindano ya vijana mwishoni mwa mwezi ujao ili kupata timu ya taifa ya ngumi ya wanawake