Katibu Mkuu TFF - Mwesigwa Celestine
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini TFF Mwesigwa Celestine amesema, kila timu inasajili kutokana na mapungufu ndani ya timu hivyo benchi la ufundi kwa kila timu yanatakiwa kuhakikisha inasajili kwa kuboresha kikosi kuelekea mzunguko wa pili wa ligi.
Kwa upande mwingine Mwesigwa amevitaka vilabu kujenga mazoea ya kukutana na kuongea linapofikia suala la klabu moja kumtaka mchezaji kutoka klabu nyingine huku akiwataka wachezaji pia kuwa wakweli katika suala la mikataba ndani ya vilabu vyao ili kuepukana na adhabu za kufungiwa.
Dirisha la usajili kwa vilabu vyote vya ligi linatarajiwa kufunguliwa kesho na litafunga Desemba 15 mwaka huu
