Sunday , 30th Oct , 2016

Bondia Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ ameonesha ni moto wa kuotea mbali linapokuja swala la kurusha ngumi baada ya kumchakaza Mchina, Chengbo Zheng katika raundi ya kwanza kwenye pambano la raundi 10 lilifanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee,Dsm.

Wakati wengi wakiamini pambano litakuwa na ushindani mkali, Dulla alishambulia kwa kasi na kumuangusha Zheng ambaye aliinuka kwa kujikongoja ambapo Dulla alimsogeza kona na kupeleka ngumi nne mfululizo ambazo zilimmaliza na kumaliza pambano kwani baada ya Zheng kwenda chini, hakuweza kuinuka tena na kushindwa kuendelea na pambano hilo.