Saturday , 27th Jan , 2018

Nahodha wa klabu ya Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC Himid Mao amesema mechi ya leo dhidi ya Yanga SC haitaweza kuwa rahisi kama wanavyofikilia kwa madai hawawezi kumkaribisha mtu kwao halafu akatoka salama.

Nahodha Himid Mao

Himid Mao ameeleza hayo ikiwa yamebakia masaa machache kuelekea  mchezo huo ambao umepangwa kufanyika katika viunga vya Azam Complex Chamanzi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam majira ya saa 10:00 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.

"Sisi kama Azam FC daima tunavyokuwa tunacheza mechi za hapa nyumbani huwa hatuna 'pressure' japo tunafahamu nini tunachotakiwa tufanye. Mechi ya nyumbani mtu tunamkaribisha lakini anatakiwa ajue haitakuwa rahisi kwake", alisema Himid Mao.

Kwa upande mwingine, Himid Mao amesema yeye na wachezaji wenzake wamejipanga vyema katika kuiwakilisha timu yao ili iweze kupata matokeo mazuri.