Friday , 20th Feb , 2015

Serikali imetakiwa kujitokeza kwa ajili ya kuwekeza katika michezo mbalimbali hapa nchini ikiwemo mchezo wa Judo.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Katibu wa Chama cha Judo Tanzania JATA, Innocent Malya amesema, timu ya Tanzania inaposhiriki mashindano mbalimbali makubwa viongozi hushindwa kuhudhuria, suala linalofanya wachezaji kukosa hamasa katika ushiriki wa mashindano hayo.

Malya amesema, Serikali inatakiwa kutenga bajeti kwa michezo inayofanya vizuri hapa nchini ili kuweza kuiongozea michezo hiyo nguvu ya kuendelea kufanya vizuri zaidi na kuweza kuipeperusha bendera ya nchi.