
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TFF, Malangwe Mchungahela.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Malangwe Mchungahela amesema fomu zaidi ya 15 za wajumbe zimeshachukua, zikiwemo huku fomu mbili za nafasi ya Makamu Mwenyekiti ambazo tayari zimeshachukuliwa.
Fomu za kuwania nafasi ya Mwenyekiti zilizochukuliwa mpaka sasa ni nne, moja ya wagombea wa nafasi hiyo ni Dk Jonas Tiboroha ambaye amewahi kuwa katibu mkuu wa timu hiyo.
''Mchakato unaendelea vizuri tu watu wanajitokeza kwa wingi na katika fomu ambazo zimeshachukuliwa, tayari 8 zimesharejeshwa na wengine wapo benki wameomba akaunti namba wanalipia wachukue fomu na kurudisha'', amesema.
Pamoja na kuwepo kwa sintofahamu ndani ya Yanga kuhusu uchaguzi huo baadhi wakitaka ufanyike wengine wakipinga lakini kamati hiyo ya uchaguzi imesisitiza uchaguzi huo upo kama ulivyopangwa kufanyika Januari 13, 2019.
Wagombea ambao wamechukua fomu.
Mwenyekiti: Jonas Tiboroha, Yono Kivela na Mbaraka Igangula
Makamu Mwenyekiti: Tito Osolo.
Wajumbe: Hamad Islam, Silvester Haule, Benjamini Mwakasonda, Salim Seif, Musa Katabaro, Shafii Amri, Said Baraka, Pindu Luhuyo, Dominic Francis, Ally Msigwa, Seko Jihadhari, Arafat Hansi, Geofrey Boniphace, Franky Ralokola, Ramadhani Said, Leonard Marango na Salum Chota.