
Kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Riadha ya Kenya Mokindo Richard, amesema tangu sheria iliyowekwa na Bunge la nchi hiyo ya kifungo cha mwaka mmoja jela na kupigwa marufuku ya kushiriki michuano miaka 4, sasa kila mwanamichezo yupo makini.
Mokindo amesema kabla ya kuja Tanzania mwezi uliopita na timu ya vijana ya nchi hiyo iliyozoa medali nyingi kwenye michuano ya Afrika Mashariki, tayari kambi ya timu hiyo ilipimwa vinasaba vya damu ili kubaini iwapo kuna utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu.