
Mchezaji mpya wa Simba Zana Coulibaly
Katika mchezo huo kocha wa Simba Patrick Aussems amefanikiwa kucheza na akili za wapinzani wake katika michuano ya klabu bingwa Afrika Nkana Red Devils ya Zambia baada ya kuchezesha kikosi ambacho hakikuwa na mchezaji hata mmoja aliyecheza mchezo wa kwanza nchini Zambia.
Kocha huyo ameanzisha kikosi cha pili akitambua kuwa wapinzani wake Nkana FC waliwakuwa na wawakilishi wao uwanjani ikizingatiwa kuwa tayari timu nzima imeshaingia nchini kwaajili ya mchezo wao wa marudiano Jumapili Desemba 23, 2018.
Hata hivyo licha ya kuchezesha kikosi hicho amefanikiwa kupata ushindi huo kupitia mabao mawili yaliyofungwa na Adam Salamba dakika ya 11 pamoja na Said Ndemla dakika ya 14 huku bao pekee la KMC likifungwa na James Msuva dakika ya 67.
Simba sasa imeendelea kubaki katika nafasi ya 3 licha ya kufikisha alama 30, ambapo ipo nyuma ya Azam FC yenye alama 40 na Yanga yenye alama 44. KMC imebaki nafasi ya 9 ikiwa na alama 17 kwenye mechi 17.