Thursday , 25th Feb , 2016

Klabu ya soka ya Al Ahly ya Misri imemtangaza aliyekuwa kocha wa zamani wa klabu za Ajax, Hamburg SV na Totenham Hotspurs Matin Jol kuwa kocha mpya klabuni hapo.

Kocha mpya wa mabingwa wa kihistoria wa klabu bingwa barani Africa Martin Jol.

Jol raia wa Uholanzi ametua klabuni hapo kutwaa mikoba ya kocha wa muda klabuni hapo Zizo ambaye naye alichukua nafasi ya mreno Jose Peseiro aliyepata kibarua katika klabu ya FC Porto.

Kocha huyo mwenye uzoefu anakumbukwa kwa mafanikio ya kuifikisha Totenham Hotspur robo fainali ya Europa league msimu wa mwaka 2006-07 na kumaliza msimu katika nafasi ya tano katika ligi kuu nchini Uingereza.

Al Ahly ambao ndio mabingwa wa kihistoria wa ligi ya mabingwa barani Afrika wanawania kurejesha hadhi yao iliyopotea misimu miwili iliyopita na mpaka sasa wanakamata usukani wa ligi kuu nchini mwao wakiwa na pointi 51 wakifuatiwa na mahasimu wao Zamaleki wanaonolewa na kocha wa zamani wa West Ham United, Alex Mcleish, wenye pointi 38 .