
Mohamed Kiganja
Akizungumza na Hot Mix Michezo Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo nchini BMT, Mohamed Kiganja amesema, hawapingi mabadiliko lakini vilabu au vyama haviruhusiwi kubadili jina lake lililosajiliwa bila kupata idhini ya msajili kwani kufanya hivyo ni kuharibu taratibu halali zilizowekwa na serikali katika kusimamia maendeleo ya michezo nchini na kunaweza kusababisha vurugu au chuki ya wananchi dhidi ya serikali yao.
Kiganja amesema, hivi sasa vilabu vya michezo vina wanachama wengi, hivyo katika suala zima la mabadiliko linatakiwa kuwahusisha wanachama wote ili kuangalia kama watakubaliana nalo ndipo masuala ya sheria yafuate.