Monday , 20th May , 2019

Kuelekea mchezo wa Ligi kuu soka Tanzania bara kati ya Singida United dhidi ya Simba, msemaji wa Simba Haji Manara amewaalika mashabiki wa klabu hiyo katika mikoa ya kanda ya kati ili waje kushuhudia timu yao ikitwaa ubingwa.

Mashabiki Simba

Akiongea leo, Manara amesema ni nafasi muhimu kwa mashabiki wa Singida na mikoa ya jirani kama Dodoma, Tabora na Kigoma kushuhudia timu yao ikicheza na Singida United katika uwanja wa Namfua.

"Ili mchezo wetu dhidi ya Sevilla uwe mzuri ni lazima kesho tushinde tuchukue ubingwa wetu kwahiyo Singida wana bahati mbaya kwetu tunahitaji kumaliza shughuli mapema" - Manara.

Klabu ya Simba tayari ipo Singida ambapo leo jioni, wachezaji wamefanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Namfua kujiandaa na mchezo huo wa kesho dhidi ya Singida United.

Simba inahitaji pointi 1 tu kutangaza ubingwa ambapo itafikisha alama 91 na kuwafanya wapinzani wao Yanga washindwe kutwaa ubingwa hata kama watazifikia pointi hizo lakini tofauti ya magoli 30 inaweza kuwakwamisha.