Monday , 27th Oct , 2014

Bondia Thomas Mashali wa Tanzania na Henry Wandera kutoka nchini Kenya wanatarajia kupanda Ulingoni Novemba Mosi mwaka huu jijini Dar es salaam katika pambano la Ubingwa wa Kimataifa la Raundi Nane.

Akizungumza na East Africa Radio, Mratibu wa pambano hilo Mabula Rushinge amesema kwa kushirikiana na Chama cha Ngumi za Kulipwa nchini TPBO wameshafanya maandalizi kwa ajili ya pambano hilo ambapo Bondia Wandera anatarajia kuwasili nchini kati ya Oktoba 28 na 29 mwaka huu.

Rushinge amesema mabondia hao wanatarajia kufanyiwa vipimo Oktoba 31 mwaka huu ikiwa ni sehemu ya mwisho ya maandalizi kwa mabondia hao kupanda ulingoni.