Monday , 18th May , 2015

Mashindano ya wazi Riadha yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 23 mwaka huu kwa kushirikisha vijana mbalimbali uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu wa Chama cha Riadha nchini RT, Suleiman Nyambui amesema, mbio hizo zitakuwa ni sehemu ya kuandaa vijana kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Riadha ya Taifa Juni tano hadi saba mwaka huu.

Nyambui amesema, mashindano hayo ya wazi yatakuwa ya mara kwa mara ili kupima uwezo wa vijana kabla ya kushiriki mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika Septemba mwaka huu nchini Congo Brazzaville.