Tuesday , 28th May , 2019

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Adi Yussuf amesajiliwa na klabu ya Blackpool  ya nchini humo kwa mkataba wa miaka miwili pamoja na kipengele cha kuongeza mkataba wa mwaka mmoja.

Adi Yussuf (katikati) akiwa na mabosi wa Blackpool

Adi ambaye amewahi kuitwa timu ya taifa ya Tanzania, amekuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na timu hiyo katika majira haya ya kiangazi.

Nyota huyo mwenye umri wa 27, anajiunga na timu hiyo inayoshiriki League One nchini England, akitokea Solihull Moors ambayo inayoshiriki National League ya nchini humo.

Amefunga magoli 21 katika michuano yote msimu huu akiwa na Solihull, magoli mawili kati ya hayo ameyafunga kwenye mechi dhidi ya Blackpool katika michuano ya FA Cup.