
Kikosi cha Yanga
Katika kikosi kilichotolewa kwaajili ya mchezo huo unaoanza saa 10:00 jioni, hakuna jina la mlinda mlango huyo namba moja pamoja na la mlinzi Kelvin Yondani ambao wanadaiwa kugoma kujiunga kutokana na kudai malipo yao ikiwemo mishahara.
Mbali na hao nyota mwingine wa Yanga Ibrahim Ajibu naye hajajumuishwa kikosi hicho wala hayupo kwenye majina ya wachezaji wa akiba hivyo hatakuwa sehemu ya mchezo huo huku akiwa hajatajwa miongoni mwa wachezaji majeruhi.
Meneja wa timu hiyo Nadir Haroub ameweka wazi kuwa wachezaji majeruhi ni Papy Tshishimbi, Juma Mahadhi na Yahya Akilimali.
Kikosi cha leo.
1. Klaus Kindoki 2. Paul Godfrey 3. Gadiel Michael 4. Andrew Vicent 5. Abdallah Shaibu 6. Feisal Salum 7. Mrisho Ngassa 8. Maka Edward 9. Heritier Makambo 10. Amis Tambwe 11. Jafari Mohamed
Akiba:
1. Ramadhabi Kabwili 2. Juma Abdul 3. Cleofas Sospeter 4. Thabaani Kamusoko 5. Raphael Daud 6. Mateo Antony 7. Yusuf Mhilu.