Friday , 28th Nov , 2014

Nchi sita zinatarajiwa kushiriki michuano ya Kanda ya tano ya mchezo wa Judo inayotarajiwa kufanyika Desemba 24 mpaka 25 mwaka huu Mjini Moshi hapa nchini.

Akizungumza na East Africa Radio,Katibu Mkuu wa Chama cha Judo nchini JATA,Innocent Malya amesema wameshatuma barua kwa vilabu shiriki katika nchi hizo ambazo ni Kenya,Burundi,Rwanda,Ethiopia,Tanzania Visiwani na wenyeji Tanzania Bara ambapo mwisho wa kutuma ushiriki ni Desemba 20 mwaka huu.

Malya amesema baada ya vilabu hivyo kuhakiki,vitaanza kuwasili nchini Desemba 21 kwa ajili ya maandalizi ambapo kuitakuwa na semina ya waamuzi na viongozi wa vilabu shiriki katika michuano hiyo.