Kocha wa Simba, Jackson Mayanja
Mayanja amesema bila nidhamu timu haiwezi kupata mafanikio hivyo kwake atakayeenda kinyume atamtimua hata kama atakuwa anaongoza katika kuisaidia Timu kufanya vizuri.
Mayanja alisema amejipanga vilivyo kuhakikisha anaimarisha nidhamu ndani ya Simba kwa faida ya timu na siyo kwa ajili yake.
Katika hatua nyingine, Manyanja alisema amefurahishwa kumuona beki wake wa kati, Isihaka kwenye kikosi cha timu hiyo baada ya kumaliza kuitumikia adhabu yake ya kusimamishwa mwezi mmoja.
Kauli hiyo ya Mayanja raia wa Uganda imekuja siku chache baada ya kumtimua beki Abdi Banda aliyegoma kupasha misuli moto wakati Simba ikicheza na Coastal Union hivi karibuni kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Pia Mayanja aliwahi kumsimamisha beki wa kati Hassan Isihaka aliyehoji kuhusu kuwekwa benchi mbele ya wenzake.