
Raheem Sterling kushoto na Leroy Sane
Sterling ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya ligi kuu ya EPL kufunga katika mechi zake 6 mfululizo dhidi ya timu moja. Sterling amefunga katika mechi 6 mfululizo alizocheza dhidi ya Bournemouth.
Nyota huyo wa zamani wa Liverpool amefunga bao moja kwenye mchezo wa leo kati ya timu yake ya Man City dhidi ya Bournemouth dakika ya 56 ya mchezo huo ambao ulikuwa unaruka 'LIVE' kupitia EATV na TV1.
Naye Winga mwingine wa Man City Leroy Sane ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyetoa pasi za magoli 'Assist' nyingi zaidi kuliko yoyote kwenye EPL, tangu kuanza kwa msimu uliopita (2017/18) hadi sasa akiwa amesaidia mabao 20.
Man City sasa wamecheza mechi 14 bila kufungwa wakishinda mechi 12 na sare 2 sasa wapo kileleni wakiwa na alama 38.
Endelea kutazama East Africa Television, kusikiliza East Africa Radio na kufuatilia kurasa zetu za mitandao ya kijamii ili kujua ni mechi gani tutairusha wikiendi ijayo.