Saturday , 21st May , 2016

Kikosi cha timu ya vijana ya Taifa ya Tanzania Serengeti Boys hii leo kitashuka tena dimbani nchini India katika mchezo wake wa nne dhidi ya Malaysia.

Kocha wa Serengeti Boys Bakari Shime amesema mchezo huo utakuwa mgumu kwa upande wa vijana wake kutokana na uchovu kwani huo ni mchezo wa nne ndani ya siku saba na pia leo ni mara ya kwanza kucheza mchezo wao usiku.

Shime amesema, mchezo wao utatanguliwa na mchezo mgumu kati ya Marekani na Korea Kusini ambapo mchezo huo utatoa sura halisi ya mashindano kwani utaamua kama Tanzania itaingia katika fainali au wapambane mpaka tone laki mwisho ili kuweza kuwa katika nafasi nzuri.

Shime amesema, Malaysia ni timu nzuri japo ilifungwa na Korea na Marekani na wanaangalia mchezo huo kama fainali.

Shime amesema, mashindano hayo yanaendelea kuwajenga kwani yatasaidia hata watakapowasili nchini kuweza kujijenga zaidi kwa kuendelea kurekebisha makosa na kujifunza yale yote watakayoyapata nchini India.

Marekani na Korea Kusini zote zinapointi nne na zilitoka sare na Tanzania,ambapo zote zinapointi nne huku Tanzania ikiwa na pointi tano na ikiwa na mchezo mmoja mkononi.