Tuesday , 6th Jun , 2017

Simba yaaga rasmi mashindano ya Sportpesa Super Cup katika mchezo wake wa kwanza baada ya kuiruhusu mikwaju 5 ya penati dhidi ya Nakuru All Stars uliopigwa leo katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.

Wachezaji wa Simba SC (Jezi nyekundu) wakiwa uwanjani wakikipiga na Nakuru All Stars (Jezi ya Machungwa)

Mtanange huo ulimalizika kwa sare tasa ya bila bila baada ya kuvujishana jasho kwa kwa dakika tisini na  timu ya Nakuru All Stars kuiibuka na ushindi wa magoli 5-4  kupitia mikwaju ya penati dhidi ya Mabingwa wa kombe la shirikisho Simba SC.

Kipa wa Simba Daniel Agyei ameipotezea simba penati moja baada ya kupaisha mpira usiozaa matunda kwa timu yake hivyo na kuipa Nakuru All Stars ushindi.

Kikosi cha Simba kilikuwa na wachezaji;  Kazimoto Mwinyi, Agyei Daniel, Bokungu Besala, Mwambeleko Jamal, Feston Munezelo, Mlipili Yusuf, Masoud Bakari, Mnyate Jamal, Luizio Juma, Athanas Pastory, Ibrahim Mohamed,.

Kikosi cha Nakuru All Stars kilikuwa na wachezaji hawa; Nganga Kamau, Lule Martin, Wainaina N Thomas, Mukhwana S James, Amakanti Ekmba, Siwa O Teddy, Amani Kyata, Nganga G Anthony, Nandwa S Dennis, Maina Geofrey, Kamau N Daniel

Nakuru All Stars itakutana na Gor Mahia zote za Kenya na Yanga kutoka Tanzania  inatarajiwa kukutana na AFC Leopard ya Kenya kwenye mchezo wa nusu fainali.