
Timu hizo zinakutana leo saa 2:15 usiku katika mchezo wa kukamilisha hatua ya makundi ya michuano ya Mapinduzi inayoendelea visiwanbi Zanzibar, ambapo zote zinawania nafasi ya kwanza katika kundi A.
''Huu mchezo tumeupa heshima ya kimpira, kwasababu Yanga msimu huu tumekutana nayo mara mbili tayari, walitufunga 2-1 kwenye mechi ya kirafiki na tukatoka suluhu kwenye mechi ya Ligi kuu hivyo tunahitaji kujibu mapigo kwa kushinda'', amesema Sanga.
Kwa upande mwingine Sanga ameongeza kuwa lengo lao ni kushinda mechi zote za makundi, hivyo leo wanaingia uwanjani wakiwa na lengo la kushinda. Pia amewapongeza waamuzi wa soka wa Zanzibar kwa kuzingatia ueledi na sheria 17 za soka, kitu ambacho kimefanya timu zishinde kwa haki.
Tayari timu hizo zote zimecheza mechi nne kwenye kundi A na kushinda zote hivyo kuwa na alama 12. Mshindi wa mchezo wa leo ndiye atakuwa kinara wa kundi hilo hivyo kusubiri mshindi wa pili wa kundi B kati ya Azam FC, Simba SC na URA.