
Mayanga amesema hayo wakati akitoa tathimini yake ya soka la Tanzania linavyoendelea kwa sasa nchini.
"Watanzania wamekuwa na tamaa ya kuona timu yao ya Taifa ikifanya vizuri katika michuano mbalimbali lakini hali imekuwa tofauti, badala yake tunafanya vibaya hii inatokana na kukosa mikakati iliyobora ya kuandaa wachezaji wakiwa bado wadogo kuwa na mipango makusudi ya kuandaa wachezaji katika timu ya Taifa," amesema Mayanga
Mayanga ameongeza "kama vilabu vyetu kuanzia ligi daraja la pili mpaka ligi kuu kama havitaweka juhudi kubwa ya kuandaa wachezaji wadogo bado tutazidi kufanya vibaya katika michuanombalimbali".
Kocha huyo wa timu ya Taifa ya ametoa tathimini yake ya jinsi soka la Tanzania linavyokwenda kwa sasa siku chache tu baada ya timu ya taifa ya Tanzania bara 'Kilimanjaro Stars' kufanya vibaya katika michuano ya CECAFA.