Wednesday , 5th Jul , 2017

Timu ya Taifa ya Tanzania imeshindwa kufurukuta mbele ya Chipolopolo kwenye nusu fainali ya COSAFA Cup 2017 baada ya kuchapwa magoli 4 kwa 2  katika mechi ya kuwania kufuzu fainali, mchezo uliochezwa leo huko Afrika kusini.

Mchezo uliochezwa muda mfupi uliopita Taifa Stars walianza kuongoza kwa kupata goli kupitia Erasto Nyoni ndani ya dakika 15 za mwanzo wa mchezo na baadaye kuja kusawazishwa na Brian Mwila dakika ya 43.

Hata hivyo hali kwa upande wa Taifa Stars ilizidi kuwa mbaya baada ya kukubali  Justin Shonga kutingisha nyavu dakika ya 45 na kuendeleza mashuti ambapo kati ya magoli matatu aliyoyafunga moja liilikuwa la mkwaju wa penati.

Magoli ya Tanzania yamefungwa na Erasto Nyoni dakika 15 pamoja Saimon Msuva dakika ya 84

Taifa stars wanatarajiwa kucheza  mechi ya kuwania nafasi ya mshindi wa tatu na timu itakayofungwa kwenye mchezo kati ya Zimbabwe na Lesotho ambao watacheza leo huko huko Afrika Kusini.