
Mshambuliaji huyo raia wa Burundi mchana huu amelazimika kuondoka kambini mjini Zanzibar kurejea Dar es Salaam mchana huu kwaajili ya matibabu zaidi kufuatia kusumbuliwa na homa.
Daktari wa timu hiyo Edward Bavu amesema kuwa Tambwe amekuwa akisumbuliwa na Malaria kwa takribani siku nne. "Ana malaria, kwa siku zaidi ya nne sasa amekuwa na wakati mgumu, tumelazimika kumrejesha Dar es salaam ili apate matibabu zaidi'', amesema Dr. Bavu.
Mrundi huyo amekuwa katika msimu mgumu, akianza kukaa nje tangu Agosti 2017, kutokana na maumivu ya goti kabla ya kurejea mwezi Desemba, lakini mapema leo ameoondolewa tena kambini kwa sababu ya Malaria.
Kuugua kwa Tambwe kunazidi kuipunguzia nguvu safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo ambayo pia inawakosa nyota wake Mzimbabwe Donald Ngoma na Mzambia, Obrey Chirwa.