
Mchezaji wa Tenisi
Rais wa chama cha tenisi Tanzania TTA, Denis Makoi amesema nchi zitakazo shiriki ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Comoro, Sudan, Somalia, Ethiopia, Eritrea, Ushelisheli, pamoja na Tanzania kama mwenyeji.
Aidha amesema TTA kwa kushirikiana na shirikisho la mchezo wa Tenisi Afrika (CAT) na shirikisho la Tenisi Duniani (ITF) wamejipanga vyema katika kuhakikisha mashindano hayo yanafanikiwa na timu bora kushinda, huku mazingira mazuri yameandaliwa kwa timu hizo kupata malazi mazuri kipindi chote cha mashindano.
Mashindano hayo yatahusisha vijana wa umri wa miaka 14 na 16, na washindi watapata tiketi ya kushiriki mashindano ya tenisi ya Afrika mwezi Aprili mwaka huu, katika nchi za Afrika Kusini na Morocco.
Imeandaliwa na Juma Idd kwa kushirikiana na Daimu Hassani.