Monday , 28th Jul , 2014

Rais wa TFF Jamal Malinzi amesema amelazimika kutoa onyo ama kuwakumbusha waamuzi juu ya suala hili ambalo limekuwa ni tatizo kwa muhstakabali wa soka hapa nchini na duniani kote kwa ujumla

Pichani baadhi ya waamuzi wa Tanzania waliohitimu kozi ya uamuzi ya FIFA.

Shirikisho la soka nchini TFF limewakumbusha waamuzi wa soka hapa nchini kuwa makini katika kazi yao na kujiepusha na masuala ya rushwa na upangaji matokeo

Kauli hiyo imetolewa na Rais wa shirikisho la soka nchini TFF Jamal Malinzi wakati akifunga kozi ya waamuzi wa FIFA na hivyo kuwataka waamuzi hao na wengine wote kuheshimu taaluma yao kama wanataka mchezo wa soka uendelee hapa nchini na hata wao kuepuka rungu la CAF na FIFA kutokana na adhabu kali ambayo itaambatana na kifungo jela kwa mwamuzi atakayebainika kuhusika na tabia hiyo katika mchezo wa soka

Aidha Rais Malinzi amethibitisha kuwepo kwa watu nje ya nchi wakicheza kamali kwa baadhi ya michezo ya ligi kuu ya soka Tanzania bara kitu ambacho hata CAF na FIFA wanakijua na tayari uchunguzi umeanza ili kubaini wahusika

Malinzi amesema ndiyo maana kwa kutambua hilo na kuwaepusha waamuzi wa Tanzania wameamua kuwaonya na kuwakumbusha juu ya tabia hiyo ambayo imeshamiri duniani kote kwa sasa.