
Job Ndugai.
Akiongea Bungeni leo Mei 22, 2019, Spika Ndugai amesema viongozi wa timu hiyo, wanaendelea kuratibu safari hiyo huku akiwahimiza wabunge wajitokeze kwa wingi ili wakaipe nguvu timu.
''Waziri Mkuu na Mimi tutakuwa miongoni mwa wabunge watakaokwenda Misri kuinga mkono timu hiyo, niwaombe wabunge muendelee kujiandikisha kwani gharama ni nafuu'', amesema.
Aidha Ngugai amewataka wabunge wenye nia ya kwenda kuthibitisha mapema ili hoteli watakapofikia pamoja na tiketi ziandaliwe mapema kwani TFF kwa kushirikiana na Wizara ya Habari wanaendelea kufuatilia suala hilo.
Taifa Stars inashiriki AFCON kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39 kupita tangu ilipofuzu kwa mara ya mwisho mwaka 1980. Stars ipo kundi C na timu za Senegal, Algeria na Kenya.