Monday , 29th Dec , 2014

CHAMA cha Kuogeleaq nchini TSA, kimesema kinatarajia kuchukua vijana walioshiriki mashindano mbalimbali mwaka huu na kuweza kukuza vipaji vyao ili kuweza kushiriki mashindano ya Afrika na Dunia hapo mwakani.

Akizungumza nja East Africa Radio, Katibu Mkuu wa TSA, Noel Kihunsi amesema pia wanatarajia kuwa na vijana ambao watawapata katika mashindano ya vijana hapo mwakani ili kuweza kupata bvijana wengi zaidi na kuweza kushiriki mashindano ya ndani na nje ya nchi.

Kihunsi amesema makocha wa vilabu hapa nchini wanatakiwa kuongeza juhudi kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa vijana hao ili kuongeza vipaji walivyo navyo hivi sasa.

Kihunsi amesema baadhi ya vijana ambao wapo katika vilabu vyao hapa nchini wapo mapumziko na wanatarajia kurudi katika mazoezi kama kawaida ili kuweza kuwaandaa vijana hao ili kuwa na maandalizi ya muda mrefu pamoja na maandalizi ya mashindano ya vilabu.