
Mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu hiyo Anton Kimath amesema wameamua kuchukuwa uamuzi huo kutokana na timu yao kuwa na matokeo mabovu.
Kimath amesema wanamshukuru Aluko kwa kuweza kuisaidia timu yao kupata point 20 mpaka sasa lakini ameshindwa kufikia lengo la kuinusuru timu kushuka daraja.
Kwa upande wake kocha huyo amesema viongozi wa timu hiyo wamemtoa kafara kwani ndani ya timu hiyo kuna matatizo mengi sana yanayowakabili wachezaji kama wachezaji kukosa stahiki zao kwa wakati pamoja na huduma za kiafya.
Aluko amesema kikosi cha timu hiyo kimesajiliwa kimakundi kwani kila kiongozi anawachezaji wake hali inayomuwia vigumu kupanga timu kwani kila upande ukitaka wachezaji wake ndio wapewe nafasi.
Aluko aliikuta African Sports wakiwa na point 3 baada ya kucheza michezo 8 wakifungwa 7 na kushinda mchezo 1 ambapo chini ya uongozi wake amekiongoza kikosi cha timu hiyo kwa michezo 15 akishinda michezo 4 sare 4 akifungwa 6.