
Vijana wa Mkoa wa Dar es Salaam wametakiwa kushiriki michezo ili kujipatia ajira na sikukaa vijiweni wakicheza mchezo wa pool.
Mkuu wa wilaya ya Temeke Mheshimiwa, Sofia Mjema amesema vijana wa Wilaya za Dar es Salaam wengi hawana ajira na ili kujipatia ajira hizo wangejishughulisha na michezo yenye tija kama mpira wa miguu, mpira wa wavu, mpira wa kikapu, netball na mingineyo.
Mjema amesema kama vijana wanapewa fursa za kimichezo na kusaidiwa vifaa vya mchezo huo, wangepatikana wanamichezo wengi, ambao wangeliletea sifa Taifa.
Amesema ana mikakati ya kuwakusanya vijana kwenye Wilaya yake ili washiriki michezo, na kutaka watu waliovamia viwanja vya michezo waondoke mara moja ili vijana wapate sehemu za kuchezea.