Monday , 7th Sep , 2015

Mashindano ya Mpira wa Wavu wa Ufukweni ya Mkoa wa Dar es salaam yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Oktoba 26 mpaka 29 mwaka huu jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa wavu Mkoa wa Dar es salaa DAREVA Siraju Mwasha amesema, mashindano hayo yanatarajia kushirikisha vilabu takribani 15 kutokana na idadi ya timu zitakazojitokeza.

Mwasha amesema, mashindano hayo ambayo yatasaidia kuukuza mchezo huo na kuweza kupata vipaji vipya vitakavyoweza kuunda timu ya Taifa ya mchezo huo wanaamini yatakuwa na ushindani mkubwa kutokana na baadhi ya timu zilizohakiki ushiriki kuwa katika maandalizi ya hali ya juu.

Mwasha amesema, kwa mkoa wa Dar es salaam wana timu nyingi za mchezo huo ambapo huwa na wachezaji wawili na wanatarajia mpaka kufikia muda wa mashindano hayo timu nyingi zitakuwa zimekwisha hakiki ushiriki wake.