
George Lwandamina
"Hatuwajui wapinzani wetu kwa sababu sijawaona wakicheza, kwa hiyo nitakwenda na kikosi chote kwa ajili ya kuhakikisha tunapata ushindi mzuri utakaotuweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kabla ya mechi ya marudiano," amesema Lwandamina.
Mzambia huyo amesema maandalizi yao anakwenda vizuri na wachezaji wao wote wapo fiti isipokuwa Donald Ngoma ambaye ataendelea na matibabu baada ya kuumia mchezo uliopita.
Amesema ukimtoa Ngoma waliobaki wote wapo sawa akiwepo Amissi Tambwe na Obrey Chirwa ambaye anaweza kuwa Mbadala wa Ngoma kwenye mchezo huo endapo mchezaji huyo hatokuwa fiti hadi siku ya mchezo.
Yanga inapewa nafasi kubwa ya kushinda na kusonga mbele hatua inayofuata kutokana na ubora wa kikosi chake tofauti na wapinzani wao Ngaya de Mbe, ambao licha ya kuwa mabingwa mara nne wa nchi yao lakini kiwango cha soka la taifa lao kipo chini ukilinganisha na Tanzania.