
Haji Manara
Manara ameyasema hayo kwenye mkutano na wanahabari wakati akitoa shukrani za bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo kwenda kwa wanachama wakiwashukuru kwa kufanikisha zoezi hilo bila vurugu zozote.
''Kwa dhati kabisa bodi inawashukuru wanachama wote wa Simba kwa kufanikisha mabadiliko ya mfumo na muundo wa klabu jambo ambalo limefanyika kwa mafanikio makubwa tofauti na wenzetu Yanga ambao kwasasa pamenuka, hawaeleweki wanafanya uchaguzi lini mara leo, kesho, kesho kutwa na utasikia kuna fuso la bakora limepaki pale'', amesema.
Manara amesema tayari bodi mpya ya wakurugenzi ya Simba imeshaanza kazi na amewaahidi wanachama wa timu hiyo kujiandaa kushuhudia vitu vingi vizuri ikiwemo kufanya vizuri kimataifa.
Aidha Manara amewasisitiza wanachama wa klabu hiyo kutoibeza klabu ya Mbambane Swallows ambayo wamepangwa kucheza nayo kwenye hatua ya awali ya michuano ya Klabu bingwa Afrika ambapo mchezo wa kwanza utapigwa hapa nchini kati ya Novemba 27 na 28.