Tuesday , 21st May , 2019

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera, amesema kuwa Yanga itaendelea kuwa bora hata kama mshambuliaji Heritier Makambo ataondoka klabuni hapo.

Mwinyi Zahera na Heritier Makambo

Akiongea leo kuelekea michezo miwili ya mwisho wa ligi, Zahera ameeleza kuwa tayari wana mipango ya kusajili wachezaji wazuri wa kulingana au kumzidi Makambo.

Mimi naondoka Mei 29 usiku baada tu ya mechi ya mwisho dhidi ya Azam FC, naenda kwenye kambi ya timu ya taifa na kabla sijasafiri kuna wachezaji zaidi ya 8 watakuwa wameshasaini mkataba na Yanga.

Zahera ameongeza kuwa kwasasa wapo kwenye ujenzi wa timu ya msimu ujao na anaamini timu hiyo itafanya vizuri sana msimu ujao kutokana na ubora wa wachezaji wanaowasajili.