
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Thamini Walimu, Boresha Hali zao”, yanajumuisha kanuni za msingi kuhusu ustawi wa walimu zilizopitishwa miaka 50 iliyopita kwa ushirikiano wa UNESCO na ILO), ambayo yanamulika lengo namba nne katika ajenda ya maendeleo ya “Kuhakikisha elimu bora, shirikishi na yenye usawa kwa wote.
UNESCO inasema, mfumo wa ajenda ya 2030 kuhusu elimu unaangazia umuhimu wa walimu katika utoaji wa elimu sawa na bora, na hivyo ili kufikia lengo hilo na chini ya mfumo wenye rasilimali za kutosha, ufanisi unaosimamiwa, ni lazima walimu hao wapate mafunzo ya kutosha, waajiriwe, wapewe motisha, na wawezeshwe.
UNESCO inasema maadhimisho ya mwaka huu yameangukia ndani ya ajenda ya maendeleo endelevu ya 2030 (SDG’s) iliyoafikiwa mwaka mmoja uliopita.