Dkt Hamis Kigwangalla
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee an Watoto Dkt. Hamis Kigwangala kwenye mahojiano maalumu na East Africa Television (EATV) ilipotaka kujua hatua zinazochukuliwa na serikali katika kuhakikisha haki za mtoto wa kike zinatekelezwa kwa mujibu wa sheria.
Amesema wizara yake kwa mwaka huu imetunga Sheria ya Elimu ambayo inakwenda kuzuia mtu yeyote kuoa au kumpa mimba mtoto wa kike chini ya miaka 21 na utekelezaji wake utasimamiwa na wadau mbalimbali nchini.
Kwa upande wa suala la ukeketaji unaoendelea kwa baadhi ya mikoa nchini Dkt. Kigwangala amesema tatizo hilo ni suala mtambuka ambalo linawahusisha viongozi hasa wale wa kimila na tayari wameanza kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanao wakeketa watoto wa kike, pamoja na kuanza elimu zaidi kwa watoto ili kuweza kujikinga na ukeketaji.