Vyoo vya shule katika moja ya shule Tanzania
Maradhi hayo hupelekea watoto wa kuugua ugonjwa wa saratani wawapo watu wazima.
Mtafiti Mwandamizi Mkuu kutoka kituo cha utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Tanzania NIMR Dk. Hamisi Malebo amesema, utafiti wa kisayansi unaonyesha kuwa maradhi yanayowapata kina mama katika mfumo wa uzazi ikiwemo saratani hutokana na matumizi ya vifaa visivyokidhi hali ya usafi na mazingira machafu ya choo.
Dk. Malebo amesema, ili kuwa na taifa lenye afya leo na siku za usoni ni lazima kuwakinga watoto wa kike na kina mama sambamba na kutoa elimu kwa jamii ya namna ya kuwalinda watoto wa kike hasa wawapo katika siku zao za hedhi.
Naye Mratibu wa Kampeni ya Usafi wa Mazingira kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Anyitike Mwakitalima amesema serikali imeandaa mpango wa kuzifikia shule zote za vijijini katika kuhakikisha wanafunzi wanatumia vifaa salama kwani utafati wao umebaini wanawake kutumia majani ya mgomba na magunia jambo ambalo linahatarisha afya zao.
Naye Mbunge wa Viti maalumu Mhe. Stella Alex Ikupa amesema ni vyema serikali ikashugulikia suala hilo kikamilifu na kuhakikisha kuwa watoto wa kike wanalindwa kiafya ili kuwa na uzazi salama ambao utachangia kikamilifu katika mendeleo endelevu.
