Rai hiyo imetolewa na kamishna msaidizi wa nishati anayeshughulikia umeme Mhandisi Inocent Luoga wakati timu ya wataalam kutoka wizara ya nishati na madini pamoja na wakala wa nishati vijijini walipotembelea mradi wa umeme wa nishati jadidifu katika kijiji cha Lumuli wilayani Iringa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya wakala wa nishati vijijini Dkt. Gidion Kaunda amezitaka kampuni binafsi zinazofanya kazi na wakala wa umeme vijini kubuni miradi mbalimbali ya umeme ili kusukuma mbele dhamira ya serikali ya kuharakisha maendeleo ya wananchi vijijini kwa kuwapelekea umeme.
