Monday , 18th Sep , 2017

Naibu Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangala, amesema ana uwezo mkubwa wa kuweka ulinzi madhubuti wa tunu za haki na usawa kwa wote sababu anajua umuhimu wake.

Dkt. Hamisi Kigwangala

Dkt. Kigwangala amesema hayo kwa kuandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa instagram, akielezea changamoto za umasikini alizozipitia kwenye maisha yake wakati anakua, mazingira magumu ya elimu aliyokuwa anapata, huku akilinganisha na hali ya sasa ambapo hakuna uwiano wa maisha kati ya aliyenacho na asiyenacho.

"Leo hii tuna tabaka la watu wanaotembea kilomita 10 ili kuunguza mafuta na tuna kundi la watu wanaotembea kilomita 10 kutafuta mlo mmoja wa siku. Nilisema mimi ninayafahamu haya matabaka sababu nimesoma na kuishi zama za zamani na za sasa. Nina uwezo wa kuweka ulinzi madhubuti wa tunu za haki na usawa kwa wote, kwa sababu najua umuhimu wake kwa maana huko ndipo nilipotoka", ameandika Hamisi Kigwangala.

Dkt. Kigwangala ameendelea kwa kusema kwamba vitu hivyo vimeweza kumkumbusha wakati alipokuwa anasoma hotuba yake na kusababisha kuwatoa machozi wageni waalikwa waliohudhuria kumsikiliza akitangaza nia ya kugombea nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM.

Dkt. Hamisi Kigwangala alishawahi kuthubutu kugombea nafasi ya kuwa mgombea wa urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM mwaka 2015, na kuangushwa kwenye kura za maoni na kutolewa nje ya mchakato huo.

Alichokiandika Hamisi Kigwangala instagram