Sunday , 24th Dec , 2017

Wizara ya Maliasili na Utalii imeandaa Mkutano na wadau wa sekta ya uwindaji wa kitalii kujadili mikakati mbalimbali  ya kuimarisha sekta hiyo.

Katika taarifa iliyotolewa na  Wizara ya Maliasili na Utalii imesema kuwa Mkutano huo wa wadau wa sekta ya uwindaji wa kitalii utafanyika siku ya Alhamisi Desemba 28,2017 kuanzia saa 4:00 Asubuhi katika ukumbi wa LAPF mjini Dodoma.

Aidha katika taarifa hiyo imeeleza kuwa lengo wa mkutano huo ni kujadili mikakati mbalimbali ya sekta hiyo ikiwemo azma ya serikali  kuanzisha upya utaratibu wa kutoa leseni ya vitalu vya uwindaji kitalii kwa njia ya mnada.

Katika mkutano huo wa wadau wa sekta ya Malisili na Utalii  mwenyekiti wake anatarajiwa kuwa Mhe.Dkt.Hamisi Kigwangalla,na wadau wote  katika sekta hiyo wanakaribishwa ili kujadili mikakati mbalimbali ya sekta hiyo.