
Meya Iringa Mjini Alex Kimbe, Mkuu wa Wilaya Iringa Mjini Richard Kasesela.
Mkuu huyo wa Wilaya Kasesela amesema kuwa kitendo kilichofanywa na Meya wa CHADEMA si cha kiungwana kwa kile alichokidai ni kudhalilisha taasisi za serikali kuwa zinahusika na kukamatwa kwake.
Akizungumza Mjini Iringa, David Kasesela amesema “si uungwana Meya kimbe kuanza kuituhumu serikali bila namna yoyote niwaeleze ukweli, mheshimiwa kimbe amekamatwa amepokea rushwa, kwa hiyo aiache mahakama ithibitishe.”
“Kama kweli amekataa milioni 200 za viongozi wa CCM basi angeweka mtego kama aliyowekewa yeye, ila kimsingi jambo hilo haliko kwa chama au serikali na kama alikuwa hapokei rushwa kwanini hizo fedha hakutaka ziwekwe kwenye akaunti ya benki,” amesema Kasesela.
“kiukweli katika kazi malalamiko ya rushwa kuhusu Meya nimeyapokea mengi, la huyu binti sio la kwanza,” ameongeza.
Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Iringa Meya Alex Kimbe alidai “lengo la CCM ilikuwa ni kupata Meya anayetokana na Chama Cha Mapinduzi na walipoleta hoja hiyo ikashindikana kwa sababu walikiuka kanuni, na baada ya kufeli wakaamua kuniundia tuhuma mbalimbali."
Agost 16 mwaka huu Meya wa Manispaa ya Iringa Mjini Alex Kimbe alikamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Iringa kwa kosa la kuomba rushwa ya shilingi milioni 2 kwa Mkandarasi aliyefahamika kwa jina la Nancy Nyarusi.