Thursday , 17th Jan , 2019

Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Goodluck Mlinga amesema kuwa yeye binafsi hatoweza kuunga mkono hoja ya kutokuwa na imani na kiti cha Spika, Job Ndugai kama ilivyoelezwa na baadhi ya wabunge wa upinzani nchini, wakiwa Jijini Dodoma.

Spika wa Bunge Job Ndugai

Kwa mujibu wa Mlinga, haoni shida ya Spika kudai malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya wabunge wenzao wa upinzani hazina msingi bali unalenga kufanya siasa.

Akizungumza na www.eatv.tv Mlinga amesema, "sisi kwa upande wetu hatuna shida na Spika Ndugai, hoja yao kama wana haki ya kupeleka lakini hawawezi kushinda, kwa sababu ile idadi ya wabunge haitawakubali kwa hoja zao,"

"Kama wanatoa madai ya kuwatanya wajumbe wa kama PAC na LAAC yale ni mamlaka yake Spika hawezi kupangiwa nini cha kufanya kwa sababu hata wakati akiwateua hakuna aliyemshauri", amesema Mlinga.

Jana katika mkutano wao na waandishi wa habari Jijini Dodoma, kwa niaba ya Msemaji wa Kambi rasmi ys Upinzani Bungeni, Mbunge wa Kibamba John Mnyika walieleza kuwa watafikisha hoja ya kutokuwa na imani na kiti cha spika kwa maamuzi yake kwenye kamati hesabu za serikali (PAC0, pamoja na Kamati ya Hesabu za serikali za Mitaa (LAAC).

Bonyeza Link hapa chini