
Waziri January Makamba
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Makamba amesema kuwa ameshazungumza na wakuu wote wa mikoa juu ya mkakati wa kufanikisha marufuku hiyo ya mifuko ya plastiki na kuwaahidi zawadi kwa mkoa utakaoibuka mshindi pamoja na mkoa wa pili na wa tatu.
Jana nilipata nafasi ya kuzungumza na ma-RC na ma-RAS wa Mikoa yote kuweka mikakati ya kufanikisha marufuku ya mifuko ya plastiki. Pia niliahidi motisha kwa mkoa utakaoongoza kwa kutokomeza kabisa mifuko hii ifikapo Julai 1 tutawapatia TZS 40m, wa pili TZS 30m, wa tatu TZS 10m.
— January Makamba (@JMakamba) May 15, 2019
Serikali imetangaza marufuku ya mifuko ya plastiki kuanzia Juni mosi, na kusisitiza kuwa atakayevunja sheria hiyo, atakumbana na adhabu kali.
Tazama video hapa chini.