Monday , 19th Aug , 2019

Serikali mkoani Iringa imeombwa kuweka utaratibu wa kugawa bure taulo za kike katika shule za msingi na sekondari ili kunusuru afya za wanafunzi wakike ambao wanalazimika kutumia vitambaa ambavyo si salama.

Wanafunzi wa shule ya sekondari Selebo

Ombi hilo limewasilishwa serikalini na wanafunzi wa shule ya sekondari Selebo, iliyopo katika kijiji cha Ilawa wilayani Kilolo mkoani Iringa, ambapo wamesema wakipatiwa taulo hizo itawasaidia kusoma vizuri kutokana na kuepuka usumbufu wanaopata wanapokuwa kwenye hedhi.

Imeelezwa kwamba wanafunzi hao wa kike hulazimika kutumia vitambaa ambavyo si salama, kujistiri pindi wanapokuwa katika kipindi cha mabadiliko ya miili yao, kutokana na kushindwa kumudu gharama za taulo zinazouzwa madukani.

Aidha wanafunzi wa shule hiyo ambayo ina jumla ya wanafunzi 475 kati yao wasichana wakiwa ni 244, wameomba Kampeni ya Namthamini inayoendeshwa na East Africa Television na East Africa Radio, iwafikie shuleni kwao, kama ambavyo mwaka huu tayari imefika katika shule za mikoa ya Arusha, Manyara na Tabora.

Zaidi tazama Video hapo chini