
Naibu waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damasi Ndumbaro.
Ndumbaro ameyasema hayo wakati akichangia mada kwenye siku ya pili ya Kongamano la fursa za biashara baina ya Tanzania na Uganda, ambapo amesema, “Vita ya Kagera 1977 ilikuwa ni mjumuisho wa Waganda na Watanzania kuondoa utawala wa kidikteta wa nduli Idd Amini, nchini Uganda.
Waziri huo pia amekumbusha kuwa huduma ya TRC kutoka Dar es Salaam hadi Uganda huchukua siku tatu tu baada ya kuondolewa baadhi ya vikwazo, na reli ya kisasa ya mwendokasi ikikamilika, safari hiyo itakuwa ya siku moja, pia akahimiza Waganda na Watanzania kuunganisha nguvu zao na kuliingia soko la Sudan.
Kwa upande mwingine, Naibu Waziri huyo akaeleza masikitiko yake ya nchi za kiafrika kuendelea kutumia lugha za kikoloni kama lugha rasmi za vikao vya kimataifa, “Lugha pekee isiyo ya kabila fulani na isiyo lugha ya kikoloni ni Kiswahili, tubadilike, tuwe na lugha ya kutuunganisha, nayo ni Kiswahili.”
Amemaliza kwa kusema, “Natetea kiswahili kwa sababu sio lugha ya kabila lolote, ni lugha ya pili baada ya kiarabu katika bara la Afrika. Ni lugha ya kumi katika mlolongo wa lugha za kimataifa, hii ni silaha kubwa kwetu, tusiendelee kutukuza tamaduni za wenzetu kwa kudharau zetu''.