
Mwandishi wa Habari Erick Kabendera akiwa na Mwanasheria wake Jebra Kambole Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Kesi hiyo ilifikishwa mahakamani hapo leo Septemba 12 kwa lengo la kutajwa, ambapo wakili wa upande wa Serikali Wankyo Simon aliiambia Mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.
Wakili wa upande wa utetezi katika kesi hiyo, Jebra Kambole ameiambia mahakama kuwa mteja wao bado anaumwa mguu wa upande wa kulia kwakuwa umepooza na kushindwa kutembea vizuri.
Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu, ikiwemo kuongoza genge la uharifu, kukwepa kodi pamoja na utakatishaji wa fedha zaidi ya Shilingi milioni 173.
Kwa mujibu wa mashtaka yanayomkabili, Kabendera anadaiwa kuyatekeleza hayo kati ya Januari 2015 na Julai mwaka huu, Jijini Dar Es Salaam na makosa hayo yote hayana dhamana na ataendelea kusota rumande.