Thursday , 12th Dec , 2019

Muigizaji wa filamu na mfanyabiashara, Shamsa Ford, amesema atawa 'unfollow' Jacqueline Wolper na Wema Sepetu na atamuacha Irene Uwoya, endapo ataambiwa achague abaki na staa gani kati ya hao kwenye mtandao wa Instagram.

kutokea upande wa kushoto pichani ni Shamsa Ford, katikati ni Wolper, kulia ni Wema Sepetu.

Shamsa Ford ameeleza hayo kupitia EATV & EA Radio Digital,  baada ya kuulizwa kama atachagua mtandao gani wa kijamii kati ya Whatsapp na Instagram ambapo amesema. 

"Nitachagua Whatsapp kwa sababu karibia watu wangu wengi ninaochati nao na kuwasiliana nao wapo huko na ndipo kuna faida zaidi, pia sipendagi umbea wa Instagram naonaga kama unanichoshaga tu ila napendaga ule umbea wa 'live' kabisa" amesema Shamsa Ford.

Aidha akizungumzia kuhusu kuwaacha Wolper na Wema Sepetu, kisha kubaki na Irene Uwoya, Shamsa Ford amesema.

"Wema Sepetu, Wolper na Uwoya niwa 'unfollow' wawili abaki mmoja, wote ni marafiki zangu ila  kwangu mimi atabaki Irene Uwoya kwa sababu ni mshikaji wangu sana na tumetoka mbali sana" ameeleza.