Tuesday , 17th Dec , 2019

Kampuni ya Bonite Bottlers ambao ni wazalishaji wa Maji ya Kilimanjaro, leo Disemba 17, 2019 imefanya zoezi la ugawaji na kukabidhi zawadi kwa watu 45, ambao ni washindi wa  Pikipiki, Runinga (TV) na katoni 50 za maji kupitia droo ya pili ya shindano la shinda na maji ya Kilimanjaro.

Baadhi ya washindi wa Television katika droo ya pili ya shindano la shinda na maji ya Kilimanjaro kutoka kampuni ya Bonite Bottlers zilizotolewa siku ya Leo Mikocheni jijini Dar Es Salaam.

Zawadi hizo zimetolewa kwa washindi hao kupitia droo ya pili ya shindano hilo, ambalo limedumu kwa muda wa wiki nane lililohusisha mikoa ya Dar Es Salaam, Pwani na Morogoro.

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, Msimamizi wa Mauzo na Masoko kutoka Bonite Bottlers Joseph Semali ameeleza kuwa,

Pikipiki ambazo wamekabidhiwa washindi

"Leo hii tumefanya hitimisho la droo yetu ambayo imedumu kwa wiki 8 ambayo ilianza Oktoba 7, hadi Novemba 30, 2019, ambapo tulipata jumla ya washindi 90, kati ya hao 45 tulishawakabidhi zawadi zao ambao walipata Pikipiki, Runinga na Katoni  50 za maji kwa watu 15 kwa kila zawadi hizo" ameeleza.

Aidha msimamizi huyo ameendelea kusema "Kwa wateja wa Maji ya Kilimanjaro nawaomba waendelee kutuunga mkono, wauze bidhaa zetu za maji ya kilimanjaro na siku kampuni ikisema tunarudisha kitu fulani kwa wateja wetu, basi wao watapewa kipaumbele".