Tuesday , 4th Aug , 2020

Kufuatia tukio la Mr Blue kudondoka jukwaani kwenye tamasha alilofanya weekend iliyopita, msanii Madee ametoa wazo kwa wasanii wengine kukata bima za maisha na afya zao na sio kukimbilia kukata bima za magari kwa sababu ya kuogopa kukamatwa na traffic.

Madee upande wa kushoto, kulia ni Mr Blue

Akiandika wazo hilo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter Rais wa Manzese Madee ameeleza kuwa,  "Nimeona video Herry Samir Mr blue ameanguka jukwaani, natoa pole kwa niaba ya wanamuziki wote, Mungu akusimamie urudi tena kazini".

"Ifike muda sasa wasanii mjikatie bima za maisha yenu, msikimbilie kukatia bima magari kisa unaogopa kukamatwa na traffic, hizi ajali za majukwaani zimekua nyingi siku hizi, hela uliolipwa unaenda kujitibia ni wazo tu" ameongeza Madee.