
Msanii wa filamu Bongo Dude
Akitoa taarifa hizo kupitia EATV & EA Radio Digital Katibu wa wasanii wa filamu Jafari Makatu ameeleza kuwa, Dude alikuwa anawahi gari la wasanii ambao wanasafari ya kwenda Dodoma, alivyofika Magomeni Usalama akapata ajali iliyomsababishia majeraha kichwani.
"Kwa sasa tupo Hospitali Magomeni, alikuwa kwenye bodaboda akagongwa na Ambulance yeye na dereva wake wote wapo hospitali, amepata majeraha kichwani kwa hiyo ametoka kupiga Xray tunasikilizia majibu kama itashindikana tutamuhamishia Hospitali ya Rufaa wasanii wenzake wote wapo hapa hospitali, mwanzo alikuwa hawezi hata kuongea ila sasa hivi anaendelea vizuri kidogo" ameeleza Katibu wa wasanii Jafari Makatu
Zaidi tazama hapa chini kwenye video.